Ushindani kwenye ligi unatuimarisha - Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Nov 2019
Ushindani kwenye ligi unatuimarisha - Aussems

Wakati kikosi chake kikiwa kinaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amesema anafurahia kuona ushindani uliopo katika ligi hiyo msimu huu umeongezea na kueleza kuwa hali hiyo inaongeza umakini kwenye timu yake

Aussems amebainisha kuwa ushindani pia unasaidia kuimarisha viwango vya wachezaji kwa sababu kila mmoja anajiimarisha ili apate namba katika kikosi cha kwanza.

Aidha, ameongeza kuwa ushindani unapokuwa mkubwa, kila timu inalazimika kuongeza mbinu za kusaka ushindi kwa sababu hakuna anayeamini atapata matokeo mazuri kabla ya kuingia uwanjani

"Ushindani ni mzuri, utafanya kila mmoja afahamu hayuko mahali salama, hakuna jambo jepesi, tunajiimarisha kila siku, kwa sababu tunataka kupata matokeo mazuri, hakuna mechi nyepesi, hakuna mwenye uhakika wa kushinda nyumbani au ugenini," alisema Aussems

Mbelgiji huyo aliongeza kuwa mbali na ushindani katika ligi, pia katika kila timu kuna ushindani na hali hii inasaidia kuwafanya wachezaji "waamke" na kujipanga kupambana.

"Mechi ni ngumu, timu zimeimarika, kila upande sasa unafanya vizuri, tayari wachezaji wameimarika tofauti na tulivyoanza msimu, ili tufikie malengo, tunatakiwa kujituma zaidi," alisema kocha huyo

Alisema kuwa baada ya kuwapa mapumziko wa siku tatu, kikosi chake kimerejea mazoezini leo kujiandaa na mechi dhidi ya Ruvu Shooting, na anaamini ataendelea kuwatumia wachezaji wote waliosajiliwa kulingana na aina mpinzani wanayekutana naye

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
3h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
3h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
6h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’