Katika jitihada za kuhakikisha nahodha wa Simba John Bocco anapona haraka na kurejea kikosini, benchi la ufundi limempunguzia muda wa kufanya mazoezi
Bocco amekuwa nje kwa zaidi ya wiki 10 akisumbuliwa na majeraha aliyopata kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc ambao ulipigwa August 17
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amethibitisha kuwa Bocco atakuwa akifanya mazoezi kwa muda mfupi ili kumsaidia apone haraka
"Kwa sasa Bocco amepunguziwa mazoezi na atakuwa anafanya mazoezi kwa muda mdogo kwa sababu akifanya hivyo anapata maumivu ambayo yanamchelewesha kupona hadi sasa licha ya kwamba anahitajika ndani ya timu," Rweyemamu alinukuliwa na Championi
"Tumeona mazoezi ya muda mrefu yanachangia kumfanya hadi sasa ashindwe kurejea ndani ya timu na plani ambayo iko mbele ni hiyo, atafanya mazoezi kwa muda mchache chini ya uangalizi wa madaktari wa timu"