FIFA yamfungia Malinzi miaka 10

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Nov 2019
FIFA yamfungia Malinzi miaka 10

Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) limemfungia kwa miaka kumi (10) aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania Jamal Malinzi baada ya kumkuta na hatia ya matumizi mabaya ya fedha na kughushi nyaraka.

Mbali na adhabu hiyo, Malinzi pia amepigwa faini ya Dola za Kimarekani 503,000 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 1.1 za Kitanzania.

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Maadili ya FIFA baada ya uchunguzi uliobaini kuwa Malinzi alihusika katika matumizi mabaya ya fedha za FIFA (FIFA Financial Assistance Programme (FAP) funds), fedha za CAF, fedha nyingine za TFF pamoja na kughushi nyaraka za maazimio ya Kamati ya Utendaji ya TFF kati ya mwaka 2013 na 2017.

Adhabu hiyo inaanza kufanya kazi kuanzia Novemba 8, 2019 na tayari Malinzi mwenyewe ameshajulishwa.

"Kamati imemkuta na hatia ya kuvunja kanuni ya 24 inayohusu kughushi nyaraka, na kanuni ya 28 inayohusu matumizi mabaya ya fedha katika kanuni za maadili ya FIFA toleo la mwaka 2018 na hivyo inamfungia miaka kumi kujihusisha za shughuli zote za soka Kitaifa na Kimataifa" imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa leo na FIFA.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
30m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’