Simba imejaliwa kuwa na wachezaji wanaomudumu kucheza zaidi ya nafasi moja uwanja
Erasto Nyoni, Mzamiru Yassin na Shomari Kapombe ni miongoni mwa wachezaji hao
Kapombe amekuwa akicheza nafasi ya ulinzi wa kulia, lakini ana uwezo wa kucheza kama mlinzi wa kati, kiungo na hata mshambuliaji
Wakati Simba ikinolewa na Pierre Lechantre, Kapombe alitumia zaidi kama kiungo wa ushambuliaji
Kapombe amefichua kuwa wakati anaanza soka alikuwa mshambuliaji
"Nilianza maisha ya soka kama mchezaji wa nafasi za mbele, nikiwa timu ya U14 nilikuwa nacheza kama mshambuliaji mpaka nakwenda U17 bado nilikuwa nacheza nafasi ya ushambuliaji," amesema
"Lakini baada ya mmoja wa mchezaji wetu kuondoka kikosini, kocha akanibadilishia majukumu akitaka nicheze nafasi ya kiungo"
"Alinipa mbinu na maelekezo ya kuweza kufanikiwa katika nafasi hiyo. Nakumbuka Mazoezi yalikuwa yanaanza saa 9 kocha akawa ananiambia nifike uwanjani saa 8 nilikuwa nafika saa 8 ananifundisha na vitu vingine ananiandikia, vitu hivyo hadi leo vinanisaidia"
Kapombe ameanza kurejea kwenye ubora wake baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa miezi saba
Hivi karibuni alitangaza kustaafu kuchezea timu ya Taifa akihitaji muda zaidi ya kuimarisha afya yake