Kanda afurahia maisha Msimbazi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Nov 2019
Kanda afurahia maisha Msimbazi

Mshambuliaji wa Simba Deo Kanda ameeleza kufurahia maisha ndani ya kikosi hicho kilichomsajili kutoka klabu ya TP Mazembe

Kanda alitua Simba mwanzoni mwa msimu kwa mkopo wa msimu mmoja akitoka Mazembe

Mshambuliaji huyo mkongwe, katika mchezo dhidi ya Mbeya City alifunga bao lake la kwanza msimu huu akiisaidia Simba kuondoka na ushindi wa mabao 4-0

Amesema tayari ameanza kuzoea mazingira ya Tanzania jambo ambalo litamsaidia kufanya vizuri zaidi

"Maisha ni mazuri na siku zinavyokwenda ndivyo nazoea mazingira ya Tanzania. Jambo hili linazidi kuniongezea ufanisi katika kutimiza wajibu wangu," amesema

Aidha mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya DR Congo, amesema ligi ya Tanzania ina ushindani, timu ndogo zinaonyesha ushindani mkali

"Nimejifunza timu za hapa zina ushindani hakuna kubwa wala ndogo, jambo kubwa ni kupambana na kufanya kazi ili kuwapa furaha mashabiki"

Kutokana na upana wa kikosi cha Simba, kocha Patrick Aussems amekuwa akimpa Kanda nafasi kulingana na mahitaji ya mchezo

Uwepo wa nyota kama Ibrahim Ajib, Francis Kahata na Miraji Athumani umepelekea asiwe na nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’