Huu ni mwanzo, mazuri zaidi yanakuja - Sheva

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Nov 2019
Huu ni mwanzo, mazuri zaidi yanakuja - Sheva

Mshambuliaji anayekuja kwa kasi kunako klabu ya Simba Miraji Athumani,  ametamba kuwa bado hajaonyesha kiwango kile kikubwa anachokitaka yeye huku akiahidi kuifanyia makubwa timu yake hiyo mpya ikiwemo kuubakisha ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Kauli hiyo ameitoa siku chache baada ya kutoka suluhu na Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Miraji maarufu kama 'Sheva' hakuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo kilichoivaa Prisons kutokana na majeraha

Msimu tayari amefunga mabao manne huku akisababisha penalti tatu na ametengeneza bao moja.

Sheva alisema anaamini bado ana imani kubwa ya kuendelea kuwatengenezea nafasi za kufunga wachezaji wenzake, pia yeye mwenyewe kufunga mabao kutokana na malengo aliyojiwekea.

Sheva alisema anafurahia ushirikiano mkubwa anaopata kutoka kwa wachezaji wenzake mara baada ya kutua Simba kwenye msimu huu wa ligi akitokea Lipuli FC ya Iringa.

"Kila mchezaji ana malengo yake aliyojiwekea, kama mimi baada ya kujiunga na Simba ninafikiria kuifanyia mengi mazuri ikiwemo kuipa ubingwa wa ligi na Kombe la FA, hivyo suluhu waliyoipata na Prisons siyo sababu ya wao kupoteza matumaini ya kutwaa mataji hayo.

"Hivyo, kama mshambuliaji nitapambana kuhakikisha ninatengeneza nafasi za kufunga, pia mimi mwenyewe kufunga mabao kwa kila nafasi nitakayoipata uwanjani.

"Ninafurahia sapoti kubwa niliyoipata mara baada ya kujiunga na Simba, kwani nimekuwa nikipata pongezi nyingi na kupewa maneno ya kunipa moyo, hivyo ninajisikia furaha kuwa hapa," alisema Sheva.

GPL

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’