Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ametaja sababu ya kumuweka nje kiungo Mzamiru Yassini kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons juzi ambao ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Aussems amesema alimpa kiungo huyo mapumziko baada ya kucheza mfululizo
"Mzamiru alicheza mechi zote tano tulizocheza kabla, niliona ni wakati muafaka kumpumzisha hasa baada ya Mkude (Jonas) kurejea," alisema
Aidha Aussems amesema mshambuliaji Miraji Athumani alikuwa majeruhi ndio maana hakuwemo kabisa kikosini
"Miraji alikuwa majeruhi hivyo asingeweza kucheza"
Matokeo ya suluhu ya bila ya kufungana dhidi ya Prisons hayakuwafurahisha mashabiki wengi ambao baadhi walihoji kukosekana kwa nyota hao ambao wamefanya vizuri michezo iliyopita
ADVERTISE HERE