Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amewapa wachezaji wake mapumziko ya siku mbili baada ya mchaka-mchaka wa kucheza mechi tano
Akizungumza baada ya program ya mazoezi mepesi yaliyofanyika uwanja wa Gymkhana jana, Aussems alisema wachezaji wake wamecheza mfululizo hivyo wanahitaji mapumziko
"Tuna mechi Novemba 24, hivyo tutakuwa na muda wa kutosha kujiandaa. Nimewapa wachezaji mapumziko ya siku mbili baada ya kucheza mechi tano"
"Baadhi ya wachezaji wanakwenda kujiunga na timu za Taifa lakini wengine tutaendelea na mazoezi Jumatatu," alisema
Simba itarejea dimbani baada ya mapumziko ya mechi ya Kimataifa ambapo Novemba 24 itarejea uwanja wa Uhuru kuchuana na Ruvu Shooting
ADVERTISE HERE