Ajib anaamini ubingwa uko palepale Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Nov 2019
Ajib anaamini ubingwa uko palepale Simba

Pamoja na kupoteza alama tano katika mechi tatu zilizopita, kiungo fundi wa Simba Ibrahim Ajib amesema kwa ubora wa kikosi chao, watafanya vizuri na hata kutetea ubingwa kwa msimu wa tatu

Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Mwadui Fc kwa kufungwa bao 1-0, Simba ilimaliza hasira zake kwa kuifumua Mbeya City mabao 4-0

Jana ikapunguzwa kasi baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Tanzania Prisons hivyo kuambulia alama nne kutoka michezo mitatu ya mwisho

Lakini mwenendo huo haumpi wasiwasi Ajib ambaye jana alikuwemo kwenye kikosi kilichoikabili Prisons

"Sare ni matokeo ya mchezo, tulijipanga kupata ushindi lakini matokeo yamekuwa tofauti. Lakini hatukati tamaa bado kuna michezo mingi, naamini tutafanya vizuri," amesema

Msimu uliopita wakati akiitumikia Yanga, Ajib ndiye aliyekuwa kinara wa kutengeneza mabao ambapo alimaliza msimu akiwa ametoa pasi 17 za mabao huku mwenyewe akifunga mabao saba

Hali imekuwa tofauti tangu alipotua Simba,  mpaka sasa ametoa pasi tatu za mabao huku akiwa bado hajazifumania nyavu

Ajib amefafanua kuwa pamoja na ushindani wa namba, mbinu zinazotumiwa na kocha Patrick Aussems ni tofauti na mbinu alizokuwa akitumia Zahera wakati yuko Yanga

"Wakati tupo Yanga tulikuwa tukitumia mipira mirefu zaidi, ndio maana hata mabao mengi ambayo tulikuwa tukifunga yalitokana na pasi ndefu"

"Lakini hapa Simba ni tofauti, tunacheza pasi fupi fupi na tunatengeneza nafasi kupitia mfumo huo. Namini nitaweza kufanya vizuri pia, kikubwa nitaendelea kujituma ili kocha azidi kuniamini na kunipa nafasi ya kucheza mara kwa mara"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’