Sare isivuruge utulivu Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Nov 2019
Sare isivuruge utulivu Simba

Baadhi ya mashabiki wa Simba wameonyesha kuchukizwa na matokeo ya suluhu ya bila kufungana ambayo Simba ilipata jana dhidi ya Prisons

Simba haikuwa na mchezo mzuri sana hasa kipindi cha kwanza, ambapo pamoja na kumiliki mpira kwa muda mwingi wachezaji hawakuwa na uharaka katika kushambulia

Aidha ni mchezo ambao Simba wangeweza hata kufungwa kama Prisons waliokuwa hatari kwenye mashambulizi ya kushitukiza wangekuwa makini

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems, alisema pamoja na makosa machache yaliyofanywa na wachezaji wake, Prisons nao wanastahili pongezi kwa kuwa walicheza vizuri

Alisema mpira wa miguu ndivyo ulivyo, kuna wakati unaweza kukutana na changamoto za aina tafauti ambazo kimsingi zitakusaidia kujiboresha zaidi

Nadhani ni vyema mashabiki tukakubali kuwa nyakati hazifanani, wakati mwingine mambo yanaweza kwenda kinyume na vile tunavyotarajia

Ni kikosi hikihiki kimepata ushindi katika michezo iliyipita, kutopata ushindi jana ilikuwa bahati mbaya

Pia kuidharau Tanzania Prisons ambayo msimu huu bado haijafungwa, sio sahihi

Pengine mchezo wa jana ulizikutanisha timu mbili ambazo zimekamilika maeneo tofauti

Safu ya ushambuliaji ya Simba ilikutana na safu bora zaidi ya ulinzi kwenye ligi mpaka sasa

Aussems ameyaona mapungufu ya timu yake, bila shaka atatumia kipindi cha mapumziko ya michuano ya Kimataifa kufanya maboresho

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’