Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amewapongeza Tanzania Prisons kwa mpango walioingia nao kwenye mchezo wa jana ambao uliwawezesha kuondoka na alama moja
Akizungumza baada ya mchezo huo, Aussems alisema pamoja na timu yake kumiliki mpira kwa muda mrefu safu ya ulinzi ya Prisons ilikuwa imara kuziba njia huku wakiwa hatari kwenye mashambulizi ya kushitukiza
"Unajua sishangai kwa nini timu hii bado haijafungwa msimu huu kwa sababu wako imara sana. Walikuja hapa na lengo la kuzuia, kutunyima nafasi lakini wakitumia mashambulizi ya kushitukiza"
"Pamoja na kuwa na mpira kwa muda mwingi, tulijaribu kupeleka mipira upande wa kulia na kushoto lakini nakiri leo (jana) walitupa wakati mgumu kutengeneza nafasi"
"Tangu nianze kufanya kazi hapa Tanzania, hii ni mara yangu ya kwanza kukutana na timu inayocheza aina hiyo ya mpira, wanazuia na kushambulia kwa kushitukiza"
"Sio mbinu ambayo mimi huipendelea sana lakini nawapongeza kwa kuwa imewasaidia kupata alama moja dhidi yetu"