Mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya mabingwa watetezi Simba dhidi ya Tanzania Prisons umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Kwa mara ya kwanza msimu huu Simba imepoteza alama mbili kwenye uwanja wake wa nyumbani
Mabingwa wa nchi leo hawakuwa na mchezo mzuri sana. Lakini pia Tanzania Prisons wanastahili pongezi kwa kuonyesha upinzani mkali

Alama moja sio haba, inafanya Simba ifikishe alama 22 na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi
ADVERTISE HERE