Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere bado anaongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu msimu huu akiwa na mabao nane
Kagere leo atakuwa na nafasi ya kuongeza mabao pale atakapokiongoza kikosi cha Simba kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons
Paul Nonga wa Lipuli Fc ndiye anayemfuatia Kagere akiwa amefunga mabao sita
Aidha, Daruesh Saliboko wa Lipuli Fc jana alifunga hat-trik kwenye mchezo dhidi ya Singida United hivyo kufikisha mabao matano
Lakini pia Miraji Athumani anaendelea kuwa miongoni mwa washambuliaji wenye mabao mengi msimu huu akiwa amefunga mabao manne
Wengine wenye mabao manne ni Peter Mapunda (Mbeya City), Yusuf Mhilu (Kagera Sugar) na Ditram Nchimbi wa Polisi Tanzania
ADVERTISE HERE