Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo wanaendelea na kampeni ya kusaka ubingwa wa tatu mfululizo watakapo-wakabili Tanzania Prisons katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru jioni
Simba ndio vinara wa ligi wakijikusanyia alama 21 baada ya kushuka dimbani mara nane
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wamejiandaa kikamilifu, wakiwa na malengo ya kuendeleza wimbi la ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa
Aidha hakuna majeruhi wapya, hivyo Aussems atakuwa na kikosi chake kamili
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao katika mchezo ambao utapigwa kuanzia saa kumi kamili jioni
ADVERTISE HERE