Kiungo fundi wa Simba Sharaf Shiboub ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Sudan ambacho kitacheza michezo miwili ya kufuzu AFCON 2021 dhidi ya Sao Tome (13 / Novemba) na Afrika Kusini (17 / Novemba)
Shiboub anaungana na nyota wengine tisa wa Simba ambao mwishoni mwa wiki wataondoka kwenye kujiunga timu za Taifa
Meddie Kagere anaelekea Rwanda wakati Clatous Chama anaelekea nchini Zambia
Gadiel Michael, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Miraji Athumani na Hassan Dilunga wao watajiunga timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'
Simba imetoa nyota 10 timu za Taifa
ADVERTISE HERE