Afisa Habari wa Simba Haji Manara amewataka wachezaji wa timu hiyo kuwapa furaha mashabiki wao kesho kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons
Manara amesema ili kudumisha amani na utulivu uliopo Simba, ni muhimu kwao kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika kila mchezo wanaoshuka dimbani
"Ili tumuweke salama kocha wetu, tuwaweke salama nyie na sisi waajiriwa wengine wa Simba, chezeni kama mnacheza timu mabingwa wa nchi," amesema
"Lakini pia nawaomba mashabiki mjitokeza kwa wingi uwanja wa Uhuru kesho ili tutafute alama tatu pamoja"
Awapa somo Yanga
Katika hatua nyingine Manara amewataka mashabiki na viongozi wa Yanga kuacha kugombana baada ya timu hiyo kumtimua kocha wao Mwinyi Zahera
Manara amesema kazi kubwa ya makocha kote duniani ni kuajiriwa na kufukuzwa hivyo ni jambo la kawaida
"Nawaomba sana ndugu zetu watulie, hawa makocha wapo kwa ajili ya kuajiliwa na kufukuzwa kama tulivyo wafanyakazi wengine"
"Msianze kugombana kisa kocha kafukuzwa, mkihofia sijui alikuwa akitulipia hiki, anatufanyia hiki.."
"Kwani sisi tumeshafukuza makocha wangapi?, Tulieni hivyo hivyo dawa iwaingie taratibu kwani mkijitingisha sindano itavunjika...!"