Mlinda lango namba moja wa Simba Aishi Manula ameachwa tena katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kilichotangazwa leo na kocha Etienne Ndayiragije kwa ajili ya michezo ya kusaka tiketi ya fainali za Afcon 2021 dhidi ya Equatorial Guinea na Libya
Hata hivyo Ndayiragije amewajumuisha wachezaji saba wa Simba katika kikosi hicho kinachoundwa na nyota 27
Gadiel Michael, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Miraji Athumani na Hassan Dilunga wote wamejumuishwa katika kikosi hicho

ADVERTISE HERE