Watani wamemfurusha Zahera

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Nov 2019
Watani wamemfurusha Zahera

Yanga imetangaza kumfukuza kocha wake Mwinyi Zahera pamoja na kuvunja benchi lote la ufundi baada ya mfululizo wa matokeo mabaya

Zahera amedumu katika timu hiyo kwa msimu mmoja tu

Juzi Yanga ilifumuliwa mabao 3-0 na Pyramids Fc kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho na kutolewa kwenye michuano hiyo kwa kufungwa jumla ya mabao 5-1

Matokeo hayo pamoja na mwenendo wa kusuasua wa timu hiyo kwenye ligi, umechangia Mcongomani huyo kutimuliwa

Huu ni utamaduni wa vilabu hivi vikongwe, suala la matokeo ni hitaji namba moja

Haji Manara, Msemaji wa Simba aliwahi kumtabiria kocha huyo kuwa Msimu huu hatamaliza na atakuwa na bahati kama hawatamuondoa kwa kumcharaza viboko

Siku za karibuni mashabiki wa Yanga walionyesha hasira zao kwa kocha huyo mzungumzaji sana ambapo mkoani Mwanza baada kufungwa na Pyramids Fc, mashabiki walimpopoa kwa mawe na chupa za maji

Charles Mkwasa ameteuliwa kuwa kocha wa muda wa timu hiyo

Wakati wao wakifukuzana, Simba inaendelea kutakata hesabu zikiwa sawa kuelekea ubingwa wa tatu mfululizo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’