Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu hatimaye taarifa ni kuwa beki wa Simba, Shomari Kapombe anatarajiwa kurejea uwanjani Januari mwaka 2018.
Tangu asajiliwe Simba mwanzoni mwa msimu huu akitokea Azam FC, Kapombe ambaye ni beki hajafanikiwa kucheza katika mchezo wowote kutokana na kuwa majeruhi.
Mbali na kuwa nje pia hivi karibuni Kapombe aliingia katika mvutano na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe kutokana na kiongozi huyo kunukuliwa akidai kama Kapombe ameshindwa kucheza ni bora aondoke klabuni hapo.
Tamko hilo lilimfanya Kapombe kuja juu na kumjibu kiongozi huyo hali ambayo ilifanya kuwe na majibizano kwa siku kadhaa.
Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa, Kapombe anatarajia kuanza mazoezi mapema mwezi Januari baada ya kukaa nje kwa muda mrefu.
Aidha, Manara amewaomba mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao katika mechi yao dhidi ya Ndanda na nyingine zinazofuata licha ya kutolewa kwenye Kombe la FA.

ADVERTISE HERE