Kiungo bora wa ukabaji nchini Jonas Mkude bado hajarejea kwenye kikosi cha kwanza Simba tangu alipokamilisha majukumu ya timu ya Taifa nchini Sudan
Mkude alirejea akiwa na majeraha hivyo kuhitaji muda zaidi kuweza kukaa sawa
Hata hivyo nyota huyo anaweza kurejeshwa tena kwenye kamati ya Nidhamu kujadiliwa, safari hii ikiwa ishu kuchelewa mazoezini
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems anadaiwa kukerwa na tukio la nyota huyo kuchelewa mazoezini mara kwa mara licha ya kuonywa
Mkude ndiye mchezaji 'nguli' zaidi kwenye kikosi cha Simba, akiwa Msimbazi kwa zaidi ya miaka saba
Amekuwa akikabiliwa na changamoto ya matukio ya hapa na pale
Pamoja na ukongwe wake kwenye timu, makocha wamekuwa wakikwepa kumpa unahodha kutokana na matukio hayo
Lakini bado Mkude anabaki kuwa moja ya viungo bora kuwahi kutokea katika ardhi ya Tanzania