Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amewataka wachezaji wa timu hiyo wasibweteke na matokeo mazuri wanayoyapata
Aussems amesema bado wana safari ndefu ya kutetea ubingwa wao hivyo hawapaswi kujisahau
"Tuna timu nzuri, mafanikio yanaonekana kutokana na matokeo mazuri tunayoendelea kupata lakini bado safari ndefu," amesema
"Unaweza kudhani Simba itatetea ubingwa kwa urahisi lakini si kweli. Hatupaswi kuwadharau wapinzani wetu na kudhani tutashinda kila mchezo kwa urahisi"
"Matokeo tuliyopata mkoani Shinyanga ni ishara kuwa pamoja na ubora wa timu yetu, tunapaswa kuwa makini, matokeo mazuri ndio yatatupa ubingwa na si vinginevyo"
Baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mbeya City jana, Simba inaendelea na maandalizi ya mchezo unaofuata ambao ni dhidi ya Tanzania Prisons
Mchezo huo utapigwa Alhamisi, Novemba 07 2019