Beki Yusufu Mlipili ni mmoja wa wachezaji waliokuwa kwenye kikosi cha Simba msimu uliopita ambao hivi karibuni wamekabidhiwa zawadi ya Bodaboda na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bilionea Mohammed Dewji 'Mo'
Baada ya Simba kutetea ubingwa wa ligi kuu na kutinga robo fainali michuano ya ligi ya mabingwa, Mo aliahidi kutoa zawadi ya Bodaboda kwa kila mchezaji
Mo aliwashauri wachezaji kuzitumia Boda hizo kibiashara ili ziweze kuwaongezea kipato
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Mlipili ameonyesha Bodaboda yake huku akimpa shukrani nyingi Mo
"Asante sana bosi Mo...," aliandika Mlipili

ADVERTISE HERE