Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amewapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Mbeya City jana katika mchezo wa ligi kuu
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo uliopigwa uwanja wa Uhuru, Aussems alisema timu yake ilistahili kupata ushindi mnono
"Tulitengeneza nafasi nyingi, kama tungezitumia vyema tungeondoka na ushindi mnono zaidi," alisema
"Hata hivyo ushindi huu sio haba, nimefurahishwa na jinsi wachezaji wangu walivyocheza, tulitawala mchezo"
"Matokeo haya yanadhihirisha kuwa mchezo dhidi ya Mwadui Fc tulipoteza kwa bahati mbaya. Tunahitaji kucheza hivi Alhamisi dhidi ya Tanzania Prisons"
Mabao ya Simba kwenye mchezo huo yalifungwa na Meddie Kagere (p), Clatous Chama, Sharaff Shiboub na Deo Kanda