Wekundu wa Msimbazi, Simba wameendeleza ubabe wao dhidi ya Ndanda FC baada ya kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa katika dimba la Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara.
Ushindi huo unaifanya Simba ifunge mwaka ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 26 sawa na Azam FC Simba ikiwa mbele kwa tofauti ya mabao.
Simba ilianza taratibu kipindi cha kwanza hata hivyo kwenye kipindi cha pili ilionyesha utulivu kwa kufanya mashambulizi ya mipango langoni mwa Ndanda kupitia mipira mirefu.
Kocha Masudi Djuma alibadilisha mfumo wa uchezaji wa Simba ambapo alitumia mabeki watatu nyuma huku Shiza Kichuya aimtumia kama beki/winga wa kushoto.
Mabao yote ya Simba yalipatikana kwenye kipindi cha pili mfungaji akiwa nahodha John Bocco 'Adebayor'.
Alifunga bao la kwanza kwenye dakika ya 52 akijitishwa kona maridadi iliyochongwa na Shiza Kichuya kutokea upande wa kulia.
Dakika nne baadae Bocco akafunga bao la pili akiwahi mpira uliopishwa na mshambuliaji Moses Kitandu kabla ya mlinda lango wa Ndanda.
Ndanda ilifanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Simba lakini uimara wa safu ya ulinzi na kipa Aishi Manula ulifanikisha Smba kuondoka na alama zote tatu mkoani Mtwara.
Huo ni ushindi wa kwanza kwa kocha msaidizi wa Simba Masudi Djuma aliyekabishiwa mikoba baada ya kutimuliwa aliyekuwa kocha Mkuu Joseph Omog.

ADVERTISE HERE