Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba leo wamemaliza hasira zao kwa Mbeya City baada ya kuifumua mabao 4-0 kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru
Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi na ilihitaji dakika nane tu kuandika bao la kuongoza kupitia mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na Meddie Kagere
Mwamuzi Athumani Lazi alitoa adhabu ya mkwaju wa penati baada ya Miraji Athumani kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari

Simba iliyokuwa katika kiwango chake bora kabisa, ilitandaza kandanda safi liliowapa wakati mgumu vijana wa Mbeya City waliokuwa wameingia na mbinu ya kujihami zaidi
Mabao mengine ya Simba yalipachikwa na Clatous Chama, Sharaff Eldin Shiboub na Deo Kanda
Ushindi huo umeendelea kuikita Simba kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 21
Aidha kinara wa mabao Meddie Kagere amefikisha mabao nane baada ya bao lake alilofunga leo
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Tanzania Prisons na utapigwa Novemba 07 kwenye uwanja wa Uhuru