Awali klabu ya Simba ilitangaza kuanza matumizi ya viwanja vyake Bunju mwishoni mwa mwezi uliopita, hata hivyo imefahamika kuwa changamoto za mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam, imevuruga mipango hiyo
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji 'Mo', amesema walilazimika kusimamisha ujenzi kwa muda kutokana na mvua hizo
Hata hivyo amesema ujenzi uko mwishoni hivyo baada ya mvua kusimama zoezi hilo litakamilishwa
Amesema Simba imedhamiria kuhamia Bunju haraka iwezekanavyo ili kuepuka gharama za kukodi viwanja
Habari njema zaidi ni kuwa uzinduzi wa viwanja hivyo huenda ukafanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk John Magufuli
Mo amesema watamualika Rais Magufuli kuzindua viwanja hivyo ujenzi ukikamilika
ADVERTISE HERE