Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo kinaendelea na mazoezi kujiandaa na michezo miwili ya ligi kuu dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons
Baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Mwadui Fc, kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wanahitaji kushinda mechi hizo zinazofuata
Mabingwa hao watetezi wataanza kwa kuikabili Mbeya City Jumapili Novemba 03, mchezo ukitarajiwa kupigwa uwanja wa Uhuru
Watacheza na Tanzania Prisons Novemba 07 katika uwanja huohuo
Simba imeendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 18
ADVERTISE HERE