Aussems awapa wachezaji mapumziko ya siku moja

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
31 Oct 2019
Aussems awapa wachezaji mapumziko ya siku moja

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amewapa wachezaji wake mapumziko ya siku moja kabla ya kuendelea na maandalizi ya michezo ya ligi kuu ya Vodacom inayofuata

Simba imerejea kutoka mkoani Shinyanga mapema leo ambako jana ilipoteza mchezo wa kwanza msimu huu kwa kufungwa na Mwadui Fc bao 1-0

Baada ya mapumziko hayo Simba itajiwinda na michezo inayofuata ambayo ni dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City

Akizungumza baada ya kuwasili kutoka Sinyanga, Aussems amesema kipigo kimewakumbusha kuwa wanahitaji kujiimarisha zaidi

Amesema kupoteza mchezo dhidi ya Mwadui ni ishara kwamba ligi haitakuwa nyepesi, wanahitaji kujipanga ili kufanya vizuri kwenye michezo yote

"Pamoja na changamoto ya uwanja, kuna makosa yalifanyika yaliyosababisha kushindwa kupata pointi tatu kama malengo yetu yalivyokuwa na tumepanga kurekebisha hayo ili kuimarika katika mechi zinazofuata.

"Matokeo ya jana yameonyesha kuwa ligi inaushindani wa kutosha, ambao kila timu iliyojipanga inaweza kupata ushindi," alisema Aussems.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’