Kiraka Erasto Nyoni amesema pamoja na kupoteza mchezo dhidi ya Mwadui Fc jana, kikosi cha Simba bado kiko imara na watafanya vizuri kwenye michezo ijayo
Nyoni aliyekuwa nahodha wa Simba kwenye mchezo huo, amesema walikosa bahati ya kufunga mabao kwani walitengeneza nafasi nyingi
"Naweza kusema tulikosa bahati kwani tulitengeneza nafasi nyingi tukashindwa kuzitumia wakati wenzetu walipata nafasi moja tu wakaitumia," amesema
"Muhimu kocha ameyaona mapungufu yaliyojitokeza, atarekebisha hivyo nina imani tutafanya vizuri kwenye mchezo unaofuata"
Simba imeendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 18
Ilianza ligi kwa kishindo, ikipata ushindi kwenye mechi zote sita za kwanza
ADVERTISE HERE