Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Mwadui Fc jana, kikosi cha Simba kinarejea jijini Dar es salaam leo kuendelea na maandalizi ya mchezo unaofuata ambao kulingana na ratiba, watacheza na Tanzania Prisons
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kutokana na kupoteza mchezo wa jana
"Tunawaomba radhi mashabiki wetu kwani najua kila mmoja alitarajia tungeibuka na ushindi, lakini haikuwa bahati yetu"
"Hatukuwa na mchezo mzuri hasa kwenye kipindi cha kwanza, Kipindi cha pili tulicheza vizuri lakini haikuwa siku nzuri kwetu"
"Tunarejea Dar es salaam kujiandaa na mchezo unaofuata"
Pamoja na kupoteza mchezo wa jana, Simba imeendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 18
ADVERTISE HERE