Kocha Mwadui Fc atamba ataisimamisha Simba, ataweza?

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Oct 2019
Kocha Mwadui Fc atamba ataisimamisha Simba, ataweza?

Kocha Mkuu wa Mwadui Fc Khalid Adam ametamba kuwa timu yake leo imejiandaa kupata ushindi dhidi ya 'Mnyama' Simba ambaye mpaka sasa ameendelea kugawa dozi kwa kila aliyekutana nae

Mwadui Fc na Simba zitachuana baadae leo katika mchezo utakaopigwa uwanja wa CCM Kambarage

Simba iko Shinyanga tangu juzi, jana ikijifua kwenye uwanja huo tayari kwa mchezo wa leo

"Tunaijua Simba, tunajua wachezaji wake wanavyocheza, tumejiandaa kuwashangaza, tumepanga kuisimamisha, tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kutushangilia katika mechi hii," ametamba Khalid

Pamoja na tambo za kocha huyo, Mkufunzi wa Simba Patrick Aussems, kama ilivyo kawaida yake hakuwa na maneno mengi zaidi ya kusema wako tayari kwa mchezo na baada ya dakika tisini mshindi atakuwa amepatikana

"Tunaamini mchezo utakuwa mzuri, lakini wenye changamoto na ushindani, hakuna mechi rahisi, timu zote zinajiandaa kusaka matokeo mazuri, na wachezaji wanajua ni nafasi yao ya kujitangaza na kuonyesha wanaweza"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
13h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
14h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
17h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’