Simba leo inakibarua kimoja cha kurudisha imani ya mashabiki wao baada ya kuondolewa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho (FA) na Green Warriors itakapowakabili wenyeji wao Ndanda FC kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Simba, inaingia uwanjani leo huku pia ikiwa imetoka kumtimua kocha wake, Joseph Omog na kuzidi kuweka hofu kwa mashabiki wao kama watapata matokeo mazuri leo.
Kocha msaidizi wa timu hiyo Masoud Djuma, ambaye kwa sasa amechukua mikoba ya kocha mkuu, amesema anafahamu changamoto iliyopo kwenye mchezo huo lakini hana hofu.
Djuma, alisema anafahamu mashabiki wanataka kuona timu inapata ushindi na amewatoa hofu kwa kuwa amekiandaa vyema kikosi chake kuelekea kwenye mchezo wa leo.
“Sio tu kwa mashabiki, hata sisi wachezaji na benchi la ufundi tunataka ushindi, tumejiandaa vizuri.., tunaenda kupambana kwa ajili ya pointi tatu, sina shaka na hilo,†alisema Djuma.
Alisema wamefanya mazoeizi yakucheza soka la kasi na kuwataka wachezaji wake kutumia vizuri kila nafasi watakayoipata.
“Kama wachezaji watafanya kile tulichokifanyia mazoezi, sio tu tutapata ushindi, lakini pia tunaweza kupata ushindi mzuri,†alisema Djuma.
“Hata hivyo ni lazima tuwaheshimu wapinzani wetu, na tujue kuwa wapo nyumbani,†aliongeza kusema Djuma.
Kocha huyo ameweka wazi kuwa hawezi kumtumia beki mpya wa timu hiyo Asante Kwasi kwakuwa ndio kwanza amesajiliwa na hajakaa na wenzake kwa muda mrefu.
Simba huwenda ikaanza kumtumia mchezaji huyo kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi

ADVERTISE HERE