Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba kiko mkoani Shinyanga ambapo baadae leo watashuka kwenye uwanja wa CCM Kambarage kuikabili Mwadui Fc katika mchezo wa ligi kuu raundi ya saba
Mabingwa hao wa nchi walitua Shinyanga juzi, jana wakafanya mazoezi yao ya mwisho kuelekea mchezo huo ambao utapigwa saa kumi jioni
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema timu iko tayari kuwapa burudani wakazi wa Shinyanga na maeneo ya jirani
Amesema walichofuata mkoani Shinyanga ni alama tatu, wamejiandaa vyema kupata ushindi
Simba vinara wa ligi kuu, wanashikilia rekodi ya kuwa timu pekee ambayo haijafungwa
Wakiwa wameshuka dimbani mara sita, wameshinda michezo yote huku mshambuliaji Meddie Kagere akiongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu akiwa amefunga mabao saba