Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema tetesi zinazozungumzwa kuhusu yeye kutakiwa na timu nyingine anazisikia lakini kwa sasa yeye ni mwajiriwa wa Simba
Aussems ameyazungumza hayo baada ya kuuliza juu ya mustakabali wake hasa baada ya kuibuka tetesi kuwa mabosi wa Nkana Fc wamewasiliana nae wakiitaka huduma yake
Aidha hivi karibuni tetesi zaidi zimeibuka kuwa klabu ya AS Vita ambayo imetinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, nayo imejiunga kuwania saini yake
"Mimi bado nina mkataba na Simba ambao utamalizika mwishoni mwa msimu. Nina makubaliano mengine na klabu ya Simba hivyo jukumu langu sasa ni kuhakikisha nakamilisha kile nichopaswa kufanya hapa," amesema
"Ndio,timu nyingine zinaweza kuwa zimevutiwa nami, siwezi kuwazuia kwani kila timu inahitaji kuwa na kocha mzuri ambaye atawapa mafanikio"
"Lakini kilichopo sasa mimi ni mwajiriwa wa Simba, siwezi kuvunja makubaliano niliyoyaafiki hapa"
Aussems amekuwa akiwindwa na timu nyingi baada ya msimu uliopita kuisaidia Simba kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa pamoja na kutwaa ubingwa wa ligi kuu
Pamoja na Simba kutolewa mapema kwenye michuano ya Afrika msimu huu, bado Simba imejipambanua kwa kuwa na kikosiΒ bora
Mpaka sasa Simba imeshinda michezo yote sita ya ligi kuu