Aussems ataja siri ya mabao ya Kagere

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Oct 2019
Aussems ataja siri ya mabao ya Kagere

Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, amefungukia siri na mbinu za mabao anayofunga mshambuliaji wake tegemeo, Mnyarwanda, Meddie Kagere.

Mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita aliumaliza akiwa mfungaji bora akifunga mabao 23, msimu huu tayari amefunga mabao saba kutoka mechi tano alizocheza

Aussems amesema kuwa mshambuliaji huyo siri yake kubwa ya kufunga ni kufuata maelekezo yake ya kumtaka muda wote atembee ndani ya 18 na 6 kwenye goli la wapinzani.

Aussems alisema lengo la kumtaka acheze umbali huo ni kwa ajili ya kusubiria makosa ya mabeki na makipa kabla ya kuyatumia kufunga mabao.

Aliongeza kuwa hilo lipo wazi hadi hivi sasa hakuna bao alilolifunga la umbali wa mita 20, yote ni ndani ya 6 na 18 kwa njia ya kichwa au kumchambua kipa, siyo shuti.

"Kagere siyo mzuri katika kukaa mpira na kupiga chenga, hilo nililiona mapema tu na ndiyo sababu ya kumtaka yeye kusubiria mipira akiwa ndani ya 6 na 18 kwa ajili ya kufunga.

"Hivyo, baada ya kugundua siyo mzuri katika kupiga chenga huku akiwa anakokota mpira nikambadilishia majukumu kwa kumpa kazi ya kutembea eneo la 6 na 18 akisubiria upungufu wa makipa na mabeki wa timu pinzani.

"Nimemtaka Kagere muda wote kutokauka maeneo hayo ya hatari akisubiria mipira kutoka kwa wachezaji wenzake, ninaendelea kumpa mbinu zaidi za kuhakikisha anaendelea kufunga, ipo programu maalum nimemuandalia," alisema Aussems.

GPL

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
54m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’