Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wameendeleza wimbi la ushindi kwenye ligi kuu baada ya kuichapa Singida United bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha
Huo ni ushindi wa sita mfululizo kwa Simba ambayo imejikita kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 18
Bao pekee la ushindi lilifungwa na Miraji Athumani kwenye dakika ya 42
Miraji amechukua jukumu la kuipa Simba ushindi leo badala ya kinara Meddie Kagere ambaye huu ndio mchezo wa kwanza ambao hakufunga bao
Miraji amefikisha mabao manne akiendelea kumfukuzia Kagere aliyefunga mabao saba
Baada ya mchezo huo, mabingwa hao wa nchi wanaelekea mkoani Shinyanga ambako Oktoba 30 watacheza na Mwadui Fc
ADVERTISE HERE