Singida United na Simba zinakutana leo kwenye mchezo wa ligi kuu unaopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha
Hata hivyo mchezo huo unafanyika baada ya kufanyika kwa Tamasha la Fiesta katika uwanja huo
Lakini pia, uwanja wa Sheikh Amri Abeid ni moja ya viwanja ambavyo sehemu yake ya kuchezea 'pitch' sio nzuri
Jana Simba ilishindwa kufanya mazoezi yake ya mwisho uwanjani hapo kutokana na kuwepo kwa majukwaa
Hata hivyo Simba imekuwa ikijiandaa kucheza katika viwanja vya aina zote na kuweza kupata ushindi
Mchezo waliocheza dhidi ya Mashujaa FC kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma ni mfano wa mazingira ambayo Simba inaweza kukabiliana nayo
Mabingwa hao wa Tanzania Bara wamepania kuendeleza wimbi la ushindi dhidi ya Singida United
Β
ADVERTISE HERE