Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kiko mkoani Arusha ambapo leo watashuka katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kumenyana na Singida United
Mabingwa hao wa nchi walitua Arusha jana ambapo jioni walifanya maandalizi yao ya mwisho mjini humo
Simba vinara wa ligi wakiwa wameshinda mechi zote tano walizocheza mpaka sasa, watakuwa na lengo kuongeza alama tatu ili waweze kuendelea kujichimbia kileleni
Meddie Kagere, kinara wa mabao akiwa amefunga katika kila mchezo, hii ni nafasi nyingine kwake kuendeleza rekodi yake dhidi ya Singida United ambayo tangu kuanza kwa msimu bado haijaonja radha ya ushindi
Singida United iko mkiani kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama tatu huku ikifanikiwa kufunga mabao mawili tu katika mechi saba walizocheza
Mchezo utapigwa saa kumi jioni na utakuwa mbashara Azam TV