Manahodha wa Simba John Bocco na Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' wanaendelea na program maalum za mazoezi mepesi ambapo sasa wanakaribia kurejea kikosini
Wakati Bocco akiwa nje kwa takribani wiki nane, Zimbwe yeye alipata majeraha wakati akiwa na timu ya Taifa iliyokuwa imekwenda Rwanda kucheza mechi ya kirafiki

Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema wachezaji hao wamepona majeraha yao, wakimaliza program hiyo wataweza kujiunga na wenzao
Rweyemamu amesema wachezaji hao watajumuishwa kwenye msafara unaoondoka mapema kesho kuelekea Arusha kwa ajili ya mchezo dhidi ya Singida United
Hata hivyo, hawatashiriki mchezo huo
ADVERTISE HERE