Senzo ataka nidhamu idumishwe Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Oct 2019
Senzo ataka nidhamu idumishwe Simba

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingiza amewataka wachezaji na Wafanyakazi wa klabu hiyo kudumisha Nidhamu ili kuiwezesha timu hiyo kufikia malengo yake

Jana Senzo alishiriki katika hafla ya utolewaji zawadi kwa wachezaji wa Simba, ahadi iliyotekelezwa na mwekezaji Bilionea Mohammed Dewji aliyewakabidhi wachezaji Pikipiki, simu za mkononi na Rice Cooker

Akitoa ufafanuzi juu ya tukio la wachezaji Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Gadiel Michael na Clatous Chama kupelekewa kwenye kamati ya nidhamu, Senzo alisema suala hilo limemalizika

Senzo alibainisha kuwa alizungumza na wachezaji hao na kufikia muafaka na hivyo hakuna adhabu zaidi

cut

"Hakuna mchezaji aliyeadhibiwa bali walisimamishwa kutokana na madai ya utovu wa nidhamu," alisema

"Nilikutana na wachezaji hao na kuzungumza nao mambo yakaisha. Niseme tu, hili si kwa wachezaji pekee kwamba ndiyo wanapaswa kuwa na nidhamu bali kwa wote ili kuisaidia Simba kwenda inavyotakiwa ili mambo yaende kwenye mstari"

Nyota hao walikuwa wakikabiliwa na tuhuma za utovu wa nidhamu baada ya kukosa safari ya kanda ya ziwa mwishoni mwa mwezi wa tisa

Wote walirejeshwa kikosini baada ya kumaliza majukumu ya kuitumikia timu za Taifa

Nyoni, Gadiel na Chama walicheza mchezo uliopita dhidi ya Azam Fc wakati Mkude alikosekana kwa kuwa alikuwa majeruhi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’