Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam Fc jana, kikosi chake kitakuwa na kazi ya kuhakikisha kinabaki kileleni mwa msimamo wa ligi ambapo wanakabiliwa na ratiba ngumu ya kucheza mechi tano katika kipindi cha siku 16
Aussems amesema haitakuwa jambo jepesi hasa ikizingatiwa mechi za mikoani zitapigwa katika viwanja vizivyo rafiki
"Wengi walikuwa wakiutazamana mchezo huu dhidi ya Azam kuwa ndio mgumu zaidi kwetu lakini si kweli. Tumecheza katika uwanja mzuri hivyo tuliweza kutimiza mpango wetu wa mchezo lakini hali ni tofauti tunapoenda kucheza viwanja visivyo rafiki"
"Nimewaambia wachezaji wangu tunakabiliwa na ratiba ngumu ya kucheza mechi tano ndani ya siku 16 lengo letu ni kuhakikisha tunaendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya michezo hiyo," amesema
Simba inatarajiwa kuelekea mkoani Arusha kuifuata Singida United ambayo imehamia huko kwa muda baada ya uwanja wa Namfua kuzuiwa na TFF
Jumapili Oktoba 27 timu hizo zitachuana kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Baadae Simba itaelekea mkoani Shinyanga ambako Oktoba 30 itachuana na Mwadui Fc