Nyoni ataja siri ya ushindi mechi dhidi ya Azam Fc

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Oct 2019
Nyoni ataja siri ya ushindi mechi dhidi ya Azam Fc

Beki kiraka Erasto Nyoni amesema ushindi wa bao 1-0 waliopata dhidi ya Azam Fc jana ni matokeo ya kujituma na kutumia vyema nafasi waliyopata

Nyoni aliyekuwa nahodha wa kikosi cha Simba kwenye mchezo huo, aliishuhudia timu yake ikiondoka na alama tatu muhimu baada ya kuibuka na ushindi wa bao la Meddie Kagere 'MK 14'

Nyoni amesema mchezo ulikuwa mgumu kwa kuwa ulikutanisha timu bora zinazotumia mifumo inayofanana

"Sisi tunacheza mpira na Azam nao wanacheza ndio maana mchezo haukuwa mwepesi. Muhimu tulifuata maelekezo ya Mwalimu na tumefanikiwa kushinda," amesema Nyoni

Simba imeendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo ikishinda mechi zote tano ilizocheza kwenye ligi

Lakini pia huo ulikuwa ni mchezo wa 16 Simba inacheza bila ya kufungwa tangu wakati wa maandalizi ya msimu nchini Afrika Kusini

Β 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’