Huyu Fraga ni Mbrazil kweli?

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Oct 2019
Huyu Fraga ni Mbrazil kweli?

Kiungo mkabaji Gerson Fraga ni kama amewanyamazisha wale waliokuwa wakitabiri kuwa yeye pamoja na Wabrazil wenzie wawili hawatafanikiwa kwenye soka la Tanzania kutokana utofauti wa mazingira ya soka la nchini na huko kwao Brazil

Lakini Fraga amezoea haraka sana mazingira ya soka la Tanzania kuliko wenzie Tairone Da Silva na Wilker

Ni kiungo asiye na mambo mengi uwanjani lakini, amekuwa akifanya kazi yake ya ukabaji vyema huku akigawa mipira bila ya kuchelewa

Aina ya mchezo alioonyesha jana dhidi ya Azam Fc ambao Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0, inadhihirisha kuwa Fraga anaweza kucheza mechi ya aina yoyote, iwe fujo au tulivu

Mchezo dhidi ya Azam Fc ulijaa ubabe na matumizi ya nguvu na akili

Hata wakati Simba ilipokwenda kucheza mechi za kirafiki mkoani Kigoma, Fraga aliwashangaza mashabiki kwani alimudu kucheza kwenye uwanja wa Lake Tanganyika

Wapo walioujiuliza na kushangaa kuwa kweli Fraga ni raia wa Brazili?

Pamoja na kuwa raia wa Brazil, sehemu kubwa ya soka lake Fraga amelicheza nje ya Brazil

Pengine hiyo inaweza kuwa sababu ya yeye kwendana haraka na aina ya soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
34m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’