Kagere awaalika mashabiki uwanja wa Taifa kuona Burudani

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Oct 2019
Kagere awaalika mashabiki uwanja wa Taifa kuona Burudani

Mshambuliaji hatari wa Simba Meddie Kagere amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi leo kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa uwanja wa Taifa kuanzia saa 11 jioni

Kagere ameanza msimu kwa 'moto' wa mabao mpaka sasa akiwa amefunga mabao sita baada ya kushuka dimbani mara nne, amesema leo uwanja wa Taifa kutakuwa na burudani ya kutosha kwa ajili ya mashabiki

"Tumejiandaa vizuri, muhimu tunaomba mashabiki wote waje kwa wingi uwanja wa Taifa watuunge mkono. Tunajua hautakuwa mchezo rahisi lakini tunajiamini na tutaweza kuondoka na matokeo mazuri," amesema

Naye Mkufunzi wa Simba Patrick Aussems amefurahia ongezeko la wachezaji waliokuwa timu ya Taifa akiamini watakuwa na mchango mkubwa kwenye mchezo wa leo

"Ukiondoa Kapombe ambaye hawezi kucheza kwa kuwa ni mgonjwa, wachezaji wengine wako katika hali nzuri kuelekea mchezo wetu dhidi ya Azam," amesema

"Najua hautakuwa mchezo mwepesi kwani Azam ni moja ya timu bora nchini Tanzania kwa sasa. Wamecheza mechi tatu na kushinda zote kama ilivyokuwa kwetu kushinda mechi zote nne"

"Utakuwa mtihani mzuri kwetu lakini tuko tayari, tunawaambia mashabiki waje kwa wingi uwanjani wapate burudani"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
20m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
18h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
21h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE β†’