Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Simba ambao ndio mabingwa watetezi, jioni ya leo Jumatano watashuka dimba la Taifa kuikabili Azam Fc mchezo wa raundi ya tano kwa Simba raundi ya nne kwa Azam Fc
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na ubora wa timu zote
Simba wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi, wamejikusanyia alama 12 baada ya kushinda mechi zote nne walizocheza
Azam Fc wanashika nafasi ya nne wakiwa na alama tisa, wao pia wameshinda mechi zote tatu walizocheza mpaka sasa
Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Azam timu hizo zilipokutana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii maalum kwa ajili ya ufunguzi wa msimu
Mchezo huo umehamishiwa uwanja wa Taifa na utapigwa kuanzia saa 11 jioni
Viingilio VIP A ni Tsh 20,000/-, VIP B Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-