Rekodi zaibeba Simba mechi dhidi ya Azam FC

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Oct 2019
Rekodi zaibeba Simba mechi dhidi ya Azam FC

Katika misimu miwili iliyopita, Simba imeweka rekodi bora ya kufanya vizuri dhidi ya Azam Fc katika michezo iliyozikutanisha timu hizo kwenye ligi

Msimu uliopita Azam Fc iliambulia alama moja tu katika mchezo wa ligi kuu mzunguuko wa pili

Kwenye mchezo wa mzunguuko wa kwanza Azam Fc ilipokea kichapo cha mabao 3-1, mabao ya Meddie Kagere (2) na nahodha John Bocco huku lile la Azam likifungwa na Frank Domayo

Ushindi pekee iliyopata Azam dhidi ya Simba ni michuano ya Kagame na kombe la Mapinduzi ambayo Simba haikuwa imeipa kipaumbele

Msimu huu tayari Azam Fc wameshachezea kichapo cha mabao 4-2 kwenye mchezo wa ufunguzi wa msimu maarufu kama Ngao ya Jamii

Rekodi hizo zinaifanya Simba iingie kifua mbele kwenye mchezo wa kesho ambao utapigwa saa 11 jioni uwanja wa Taifa

Nahodha John Bocco amesema wamejipanga kuendeleza ubabe kwa Azam, wakiweka mikakati ya ushindi

"Mimi sitacheza mechi kwa sababu bado sijawa fiti, lakini nazungumza kama nahodha, tumejipanga vizuri, wachezaji wenzangu naamini watafanya kile walichoelekezwa na mwalimu," alisema Bocco.

Simba iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikikusanya alama 12 baada ya kushinda michezo yote minne iliyocheza

Azam Fc ina alama tisa ikiwa nayo imeshinda mechi zote tatu walizocheza

Hivyo ni mchezo utakaokutanisha timu zote zenye rekodi ya ushindi wa asilimia 100 kwenye ligi msimu huu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
20m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
18h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
21h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE β†’