Azam Fc hawawezi kusahau alichowafanya kiungo fundi Sharaff Elden Shiboub kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii August 17 uwanja wa Taifa
Ndio, ulikuwa ni mchezo uliomtambulisha zaidi Shiboub nchini akifunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 4-2
Kwenye mchezo huo, Shiboub alikuwa tatizo kwa Azam Fc, aina ya uchezaji wake uliwasababishia wakati mgumu Azam Fc

Sasa Jumatano kwa mara nyingine Azam Fc watakutana na Shiboub palepale kwenye uwanja wa Taifa katika mchezo wa ligi kuu
Uongozi wa Simba umethibitisha kuwa mchezo utapigwa kwa Mkapa ukitarajiwa kuanza saa 11 jioni
Simba vinara wa ligi wakiwa wameshinda mechi zote nne walizocheza mpaka sasa, wamepania kuendeleza rekodi ya ushindi kwa asilimia 100
ADVERTISE HERE