Stars yarejea kishujaa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Oct 2019
Stars yarejea kishujaa

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imerejea leo Jumamosi, Oktoba 19, 2019 ikitokea nchini Sudan ilikata tiketi ya michuano ya CHAN baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sudan

Kocha Msaidizi wa Stars Selemani Matola amesema kilicho nyuma ya ushindi wa timu ya Taifa ni kujituma na juhudi za wachezaji kutambua umuhimu wa mchezo wao dhidi ya Sudan uliochezwa jana

Matola amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kupata matokeo mbele ya Sudan kwani mchezo ulikuwa mgumu na kila timu ilikuwa inatafuta ushindi ili kusonga mbele kwenye hatua ya Fainali ya Michuano ya Chan 2020 nchini Cameroon

"Kila timu ilikuwa na lengo moja kupata matokeo chanya  nasi pia tulikuwa tunafikiria jambo hilo, mchezo ulikuwa mgumu na ndiyo maana makosa yetu yalitufanya tuende mapumziko tukiwa nyuma, mwisho wa siku tulirekebisha makosa na tukapata ushindi.

"Mapokezi ya watanzania ni faraja kwetu na inaonyesha namna gani tumefanya kitu kikubwa kwa ajili ya Taifa hii ni rekodi kwetu na tuna kila sababu za kuwashukuru mashabiki pamoja na wadau kwa sapoti yao ya hali na mali tangu mwanzo na mpaka hapa tulipofika"

Naye Erasto Nyoni, nahodha msaidizi wa Stars, amesema kuwa ni furaha kwa mashabiki na taifa kiujumla kwa matokeo waliyopata kwenye mechi ngumu waliyocheza

"Tunafurahi na shukrani zote ni kwa Mungu kwa kuwa yeye ndiye muweza wa yote, kwa sasa ni mwanzo wa kutazama hatua nyingine kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu, kikubwa ni sapoti"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’