Baada ya mapumziko ya takribani wiki tatu kupisha michezo ya kalenda za CAF na FIFA, Ligi kuu ya Vodacom inaendelea leo ikiingia raundi ya tano
Miongoni mwa meci zinazopigwa leo, Mtibwa Sugar watakuwa ugenini kucheza na Ndanda kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara.
Mchezo mwingine ni kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Sokoine Mbeya, huku Coastal Union wakiwa wenyeji wa Mwadui, Dimba la Mkwakwani, Tanga na Namungo FC wakiwakaribidha Lipuli kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi.
Mbao itawakaribisha Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza, huku Polisi Tanzania wakiwa wenyeji wa Singida United Dimba la Ushirika Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mabingwa watetezi Simba wao watashuka dimbani Oktoba 23 kuikabili Azam Fc kwenye mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru