Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amempongeza mlinda lango Beno Kakolanya kwa kuonyesha kiwango kizuri kwenye michezo ya kirafiki aliyocheza hivi karibuni
Aussems ambaye kikosi chake kimerejea juzi kutoka Kigoma, amesema Beno alikuwa bora kwenye mechi hizo na ameendelea kuwafanya vizuri hata kwenye mazoezi
"Beno amekuwa na kiwango kizuri. Amefanya vizuri kwenye michezo ya kirafiki na anafanya vizuri mazoezini pia"
"Nadhani makipa bora wa Tanzania kwa sasa wako kwenye klabu ya Simba, ni jukumu letu benchi la ufundi kuamua nani acheze wakati gani"
"Kwa sasa Aishi Manula bado ataendelea kuwa kipa namba moja, lakini jambo muhimu Beno naye atakuwa na nafasi yake kikosini"
ADVERTISE HERE